Kipa wa Nigeria Super EagleVincent Enyema, atakosekana katika kikosi cha Nigeria, kitakachoshiriki katika mechi ya kufuzu kwa fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa 2017, dhidi ya Tanzania siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mamake.
Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh, amesema kwa sasa Enyema, amepata pigo kubwa na tumemruhusu kwenda nyumbani kwa misingi ya kibinadam.
Enyema alitarajiwa kusafiri Abuja siku ya Jumatatu, lakini alifutilia mbali safari hiyo.
Kipa wa timu ya Uingereza ya Wolves, Carl Ikeme, anatarajiwa kujaza pengo hilo katika mechi itakayokuwa ya kwanza katika timu hiyo ya Super Eagles.
Enyema, anayeichezea klabu ya Ufaransa ya Lille na mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Super Eagles, alikuwa kipa wa timu hiyo wakati ilipoicharaza Chad kwa magoli mawili kwa moja mjini Kaduna mwezi Juni mwaka huu.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top